August 7, 2019


JUMA Balinya, mshambuliaji wa timu ya Yanga amesema kuwa aanaanza kazi rasmi mbele ya Township Rollers baada ya kushindwa kutupia bao kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ua Kariobangi Sharks.

Yanga itamenyana na Township Rollers Jumamosi, uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Balinya alifunga mabao 19 akiwa na Polisi ya Uganda msimu uliopita amesema kuwa mashabiki wa Yanga wataanza kufurahia mabao yake wakati ambao atapambana na Rollers.

 “Kwanza niwashukuru mashabiki wote wa Yanga kwa kile ambacho walitufanyia katika Wiki ya Mwananchi. Walikuja kwa wingi kwa ajili ya kutusapoti jambo ambalo lilitufanya tujisikie vizuri.

“Lakini kwa matokeo ya mechi ile haikuwa jambo baya ambalo tulifanya kwa sababu ndiyo mechi yetu ya kwanza kubwa, lakini pia niwaambie kwamba ni suala la muda pekee kabla ya kuona mambo mazuri. 

"Tuna kikosi kizuri hadi sasa, ninawaahidi mtafurahi katika msimu ujao wa ligi pamoja na ligi ya mabingwa katika mchezo wetu huu na Rollers,” amesema Balinya.

Yanga ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 huku mpachikaji kwa upande wa Yanga akiwa ni Patrick Sibomana kwa mkwaju wa Penalti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic