MOHAMMED Dewji, 'Mo', Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi ndani ya Simba leo ameweka picha yake kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mshambuliaji wa kimataifa, Meddie Kagere 'MK 14'.
Jana kwenye utambulisho wa wachezaji wapya wa Simba, Mo alitambulishwa kama mchezaji mpya ambaye anacheza namba zote uwanjani kuanzia golikipa, beki, mshambuliaji na kiungo.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema: "Sasa namleta kwenu mchezaji mpya wa Simba ambaye anacheza nafasi zote, kuanzia ushambuliaji huko anafunga, golikipa, beki yeye namba zote anacheza naye ni tajiri wetu Mo,".
Baada ya kusema hivyo mashabiki wote wa Simba walishangilia kwa furaha mwanzo mwisho.
sawa
ReplyDeleteMungu awabariki sana
ReplyDelete