KASSIM
Khamis, nyota mpya wa Azam FC ambaye amesajiliwa ndani ya Azam FC akitokea
Kagera Sugar amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ushindani dhidi ya Simba
kwenye mchezo wa ngao ya jamii na wana imani ya kupata matokeo.
Azam FC
ambao ni mabingwa wa kombe la Shirikisho watamenyana na Simba ambao ni mabingwa
wa Ligu Kuu Bara, leo uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa ngao ya jamii
ambao ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa ligi inayotarajiwa kuanza Agosti 23.
Akizungumza
na Saleh Jembe, mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuifunga Simba kwenye
mchezo wa ligi wakati akiwa ndani ya Kagera Sugar, msimu uliopita alisema kuwa
nafasi ya kushinda ipo .
“Tumejiandaa vema, mbinu mpya na kali ambazo tumepewa
zinatupa matumaini makubwa kwamba tutashinda hatuna wasiwasi.
“Kama
niliwafunga wakati nipo Kagera Sugar inamaana bado nina nafasi ya kuwafunga
tena nikikutana nao, haijalishi ninacheza na timu gani kazi yangu mimi ni
mshambuliaji,” amesema Kassim.







0 COMMENTS:
Post a Comment