NYOTA wa
timu ya Simba, Meddie Kagere na Hassan Dilunga wamepania kuirejesha kwa mara ya
pili ngao ya jamii makao makuu ya Msimbazi pale Kariakao mchezo utakaochezwa
leo uwanja wa Taifa.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Dilunga amesema kuwa maandalizi yamekamilika
kinachosubiriwa ni wakati ili kutimiza malengo waliyojiwekea.
“Tuna kazi
ngumu na tunajua haitakuwa kazi nyepesi ila uhitaji wa kushinda ni mkubwa
ukizingatia kwamba msimu uliopita tulitwaa taji hili lazima tupambane kubaki
nalo tena,” amesema.
Kwa upande
wa Kagere amesema kuwa wana imani ya kupata matokeo mbele ya kikosi cha Azam FC
hivyo mashabiki wawape sapoti kwani kazi itakuwa ngumu.
Kagere na Dilunga msimu uliopita walitupia mabao 2 yaliyoipa taji la ngao ya Jamii Simba mbele ya Mtibwa Sugar.








0 COMMENTS:
Post a Comment