LIGI kuu Tanzania bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa uwanja wa Uhuru majira ya saa 10:00 jioni.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na hesabu zao ni kupata pointi tatu.
"Nimewaambia wachezaji wote wapya kwamba hakuna hata siku moja Yanga inacheza mechi nyepesi, mechi zote ni ngumu wanapaswa wapambane kupata matokeo.
"Wachezaji wote ambao hawakupata leseni za kucheza mechi za CAF wote watakuwa na nafasi ya kucheza ligi na itakuwa muda wao kuonyesha kile walichonacho kwa mashabiki kwa kuwa wako vizuri," amesema.
Miongoni mwa wachezaji ambao hawajapata leseni ya CAF ni pamoja na mlinda mlango namba moja Farouk Shikalo, mshambuliaji mwili jumba, David Molinga.
0 COMMENTS:
Post a Comment