August 4, 2019


ETTIENE Ndayiragije, Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania,amesema katika mchezo wa leo wa marudiano kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya wenyeji Kenya wataingia kwa njia tofauti.

Ndayiragije amesema mchezo uliochezwa Dar es Salaam timu ilicheza vizuri isipokuwa ilikuwa na mapungufu machache ambayo ameyafanyia kazi.

Mrundi huyo anaamini Stars itasonga mbele katika hatua inayofuata kutokana na jinsi wachezaji wanavyo pokea maelekezo yake.


 "Mechi ya kwanza tuliyocheza nyumbani tulicheza vizuri zaidi ya Kenya, kuna mabadiliko nimefanya lakini siwezi kuyasema hapa yataonekana uwanjani, matumaini ya kufuzu hatua inayofuta ni makubwa," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic