INAELEZWA kuwa beki wa timu ya Simba, Juuko Murshid yupo mbioni kujiunga na klabu ya Wydad Casablanca kwa kandarasi ya miaka miwili.
Nyota huyo anayekipiga timu ya Taifa ya Uganda Uganda inaelezwa kwa sasa yupo Morocco ili kukamilisha dili hilo.
Uongozi wa Simba ulieleza kuwa mkataba wake ndani ya Simba bado unaendelea na walimwandikia barua ya kumrejesha kwenye kikosi.
Wamemlipa fedha zake, au ndo mwendelezo wa vilabu vya bongo kuwakopa wachezaji!?
ReplyDeleteMchezaji mtoro huwa halipwi
ReplyDeleteKwa hiyo Juma Abdul na Vicent Andrew Dante wana haki ya kutolipwa kwa utoro?
DeleteMishahara ndio lakini sio pesa yao ya usajili .Juuko alitoroka kazini.Juma ,Dante nä Yondani hawajalipwa pesa zao za usajili.
ReplyDeleteMmh sheria ya Usalama na Mahusiano kazini inasema unapokosa kuonekana kazini kwako kwa zaidi ya siku 5 mfululizo unakuwa umejifukuzisha kazi moja kwa moja. Rejea kesi ya Juma Kaseja dhidi ya Yanga
ReplyDeleteTaarifa kamili za kwenye mtandao zinasema Waydad wamekubaliana na Simba kununua mkataba wa Juuko uliobakia ndani ya Simba na viongozi wa Simba wamekubali na kutoa baraka zote. Sasa waandishi wakati mwengine labda hawazifanyii kazi taarifa zao au huamua kupotosha ukweli wa mambo makusudi. Kama simba walimuandikia barua Juuko ilikuwa kabla ya kupata timu na ni outdated story. Lakini pia juuko ni mchezaji halali wa Simba na aliamua kuondoka kuhuni kwenye timu na Simba ni wastarabu la sivyo wanauwezo wa kumuadabisha juuko kisheria na akadaabika.
ReplyDelete