NYOTA watano
leo watakosekana uwanja wa Taifa ambapo wanaume 22, Simba na Yanga watakuwa
wanamenyana kutafuta mshindi wa ngao ya jamii.
Ngao ya
jamii ambayo huwakutanisha mabingwa wawili tofauti msimu huu itawakutanisha
matajiri wa Dar es Salaam, Azam FC na vigogo Simba.
Jumla ya
wachezaji watano kwa timu zote mbili wataukosa mchezo huu kutokana na
kusumbuliwa na majeruhi.
Kutoka Simba
ni Ibrahim Ajibu, Aish Manula na Wilker da Silver huku kwa upande wa Azam FC
ikiwa ni pamoja na Agrey Moris na Mudathir Yahya.
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa anatambua ugumu wa mchezo wa leo ila watapambana kupata matokeo chanya.
Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa watautumia mchezo wa leo kuandaa kikosi cha kimataifa kitakaochowamaliza Fasil Kenema ya Ethiopia.








Tengeneza hapo ni Simba na Azam Yanga ilicheza Jana na polisi na ikapara kichapo
ReplyDeleteJamani siku hizi mwandishi umekuwa siyo makini kuna makosa mengi ya kiuandishi unafanya!! Ukiangalia katika habari nyingi unazotuandika ili sisi wasomaji wako tusome hazina usahihi, para ya kwanza tu hapo umeandika mchezo wa leo ni kati ya SIMBA NA YANGA!!!!! Hii ni sawa kweli!!! Unatuangusha sana ndugu mwandishi baadhi yetu sisi ni wadomaji wa ukuruda wako kila siku na kila baada ya saa furani furani lazima tupite huku
ReplyDeleteUtakuwa umetenda haki endapo nawe pia utakuwa makini katika uandishi wako uliyechangia hapo juu. Ni'mara ya kwanza' na si 'para ya kwanza'; 'wasomaji wa ukurasa wako' na si 'wadomaji wa ukuruda wako'; 'kila baada ya saa fulani' na si 'kila baada ya saa furani furani'. Tuitendee haki lugha yetu ya Kiswahili!
DeleteSishangai yanayotokea Yanga kwenye mechi za kirafiki na za mashindano ya CAF nilishashauri huko nyuma kuwa Yanga inahitaji kuliimarisha benchi la Ufundi kuongeza ujuzi na mbinu kwani viwango vya wachezaji vinaporomoka kwa kiwango cha juu mno....uwezo wa benchi la ufundi la Yanga ni mdogo mno...na kama hatua za haraka hazitachukuliwa kuliimarisha benchi la ufundi kuna hatari sana huko mbele aibu itatokea...Mimi si tu kwamba ninatathmini mchezo wa soka kwa umahiri ninazichambua timu kutokana na mechi zinazocheza.....nilisema kuwa Yanga inahitaji kuiiga Simba kutafuta Kocha Msaidizi kutoka Ulaya au Hata Amerika Kusini au Asia au Hata Africa mwenye viwango vya FIFA....ili wachezaji waongezewe mbinu katika mashindano.....Bado Yanga wana wachezaji wazuri lakini soka wanalocheza watapata tabu wakicheza na timu zenye mbinu za kubadilisha mchezo haraka.....kwahiyo hili la kubadilisha au kuliimarisha benchi la ufundi haliepukiki
ReplyDelete