August 5, 2019


WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Serikali ya Tanzania inatambua uwekezaji wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Mohamed Dewji 'Mo'.

Mwakyembe amesema kuwa tangu zamani wamekuwa wakiwasiliana na viongozi wa Simba na kuewa taarifa ambazo zinawahusu viongozi hao.

"Serikali inatambua uwepo wa mwekezaji Mo ndani ya Simba na amekuwa bega kwa bega na viongozi wa Simba hivyo nasi tunatambua uekezaji wake na wale ambao wana hofu wasiwe nayo.

"Tunaona matokeo ambayo yapo kwa sasa ndani ya Simba ni mkubwa hivyo ni ombi langu kwa uongozi wa Simba kuandaa ripoti ambayo itatumika kwa ajili ya kuwapa mafunzo wengine kufanya hivi.

"Uwekezaji kwenye mpira ni sawa na kila timu inapaswa ifikie hatua kubwa ambayo ni maendeleo kwa kila timu nchini Tanzania," amesema.

Mwakyembe leo ameweka jiwe la msingi viwanja viwili vya Simba kwa ajili ya mazoezi vilivyopo Bunju.

1 COMMENTS:

  1. Ni Tanzania pekee mtu anapigania kufanya kitu cha maendeleo kwa wote halafu anaekewa mizengwe? Kuna watu walizoea kupiga kwenye hizi klabu halafu wanajifanya wanauchungu na klabu hizi kwa kutaka kuendelea kuwa mashamba ya bibi kwa kisingizio cha kuzibakisha Simba na Yanga kuwa klabu za wananchi? Hata Manchester United ni timu ya wananchi. Hata Chelsea ni timu ya wananchi vile vile kinachotakikana ni timu kuwa na chanzo cha uhakika cha mapato kwani mwisho wa siku timu zetu zinatakiwa kushindana Africa ambako kuna timu zenye uchumi imara zaidi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic