August 7, 2019


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hauna neno la kusema kwa sasa kwa mashabiki wake zaidi ya kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi jana uwanja wa Taifa.

Simba jana ilicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Power Dynamo na iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Mchezo huo ambao ulivuta hisia za mashabiki wengi ulikuwa na ushindani na kila timu ilipambana kutafuta matokeo chanya.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa hakuna jambo jngine la kuwaambia mashabiki na wapenzi wa Simba zaidi ya shukrani.

"Mengi makubwa ambayo mmefanya kwa kuitikia wito hakuna cha kuwaambia zaidi ya kusema asante kwa sapoti yenu na kujitokeza kwenu uwanja wa Taifa.

"Picha linaanza siku yenyewe ilikuwa ni katikati ya wiki sipati picha kama ingekuwa siku ya mapumziko namna ambavyo wana Simba wangeitikia ila yote kwa yote asanteni sana," amesema.

3 COMMENTS:

  1. Kuwaangukia au? kuwashukuru.Kuwaangukia kwani wamefanya kosa??

    ReplyDelete
  2. Kuna somo kubwa sana juu ya mashabiki wa mpira nchini.(1)Inaonesha dhahiri watanzania wana mwiitiko wa hali ya juu kuunga mkono juhudi za viongozi wao kama wanaona wanaridhishwa na kazi wanayoifanya. (2)watanzania ni watu wa kujitoa kwa kilicho chao kuhakikisha kinafanikiwa na kufikia malengo hata kama kujitoa muhanga.(3)Watanzania wanapenda kufurahia maisha hata katika hali duni ya kipato. Serikali yetu ya awamu ya tano inajitahidi vya kutosha katika kuinua hali za wananchi wake kiuchumi ila kwa maoni yangu utajiri mkubwa wa tanzanzia ni watu wake yaani rasili mali watu na kama rasili mali hii itatumika vizuri zaidi basi maajabu yatatokea Tamzania katika nyanja ya maendeleo kwa kipindi kifupi.Ukiachana na viwanda nchi kama Marekani sekta ya ujenzi hasa kwa makazi ya watu namaanisha nyumba bora za kuishi kwa watu wa kawaida kama vile apartments buildings zilichangia kwa kiasi kikubwa kuipeleka nchi hiyo kunako next level kiuchumi. Watanzania wanapenda vizuri kama kutakuwa na makazi bora ya kisasa yaliyopangika na yanayoandaliwa kwa makusudi kwa makaazi ya watu wa kawaida kwa bei ya mtanzania kulingana na hali ya kipato cha mtanzania hata kama kipo juu kidogo basi watafanya kazi kugharamia makazi hayo hapana shaka kidogo.Hasa kwa wanafamilia mpya nakusudia vijana. Serikali kupitia wizara husika ijikite zaidi Ville vile kunako public housing industry kwani bado nchi yetu ipo nyuma sana katika makazi bora ya watu. Haiwezekani hata siku moja kila mtanzania ajenge nyumba yake ila apartments building residential complex ndio mpango hata kwa kuwasukuma vijana kufanya kazi kugharamia makazi yao na kwa msukumo huu wa watanzania wanapotaka lao basi hapana shaka hakuna lisilowezakana kwa sasa. Nasema hivi kwa sababu hata Daresalaam kati kati ya jiji kuna makaazi ya watu ambayo huwezi amini kama binaadamu wanaishi ndani yake kwangu mimi tatizo serikali na sio wakaazi kwani nguvu kaazi Tanzania ipo ya kutosha hivi sasa ya kubadilisha kwa kila tunachotaka kukibadilisha. Hakuna kitu rahisi katika kujenga kitu ila hata urahisi sio maisha halisi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic