August 7, 2019


MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Romelu Lukaku atapewa adhabu na klabu hiyo Kwa kukosa mazoezi bila ruhusa.

Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akifanya mazoezi na timu yake ya zamani Anderlecht kwa muda wa siku mbili zilizopita.

Timu ambazo zinashiriki Serie A, Inter Milan na Juventus zinapigana vikumbo kupata saini ya nyota huyo ambaye hajacheza mechi za maandalizi kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Julai, United ilipiga chini dau la pauni milioni 54 kutoka Inter Milan kwa ajili ya kumpata nyota huyo.

Lukaku alijiunga na United msimu wa mwaka 2017 akitokea Everton kwa dau la pauni milioni 75 msimu uliopita alitupia mabao 12.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic