BAKARI Shime, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 'Tanzanite' amesema kuwa kikosi kipo sawa kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Afrika Kusini.
Leo Tanzanite itashuka uwanjani kumenyana na timu ya Taifa ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na Saleh Jembe, Shime amesema kuwa mchezo utakuwa mgumu ila wamejipanga kupata matokeo chanya.
"Natambua mchezo utakuwa mgumu tofauti na mingine ya mwanzo kwa kuwa hii ni hatua ya mtoano.
"Lengo letu lipo palepale kutinga hatua ya fainali na kurejea na ushindi hivyo kwa sasa tupo tayari kupambana na vijana nimewapa mbinu mpya na kali," amesema.
Mchezo wa leo utapigwa majira ya saa nane kwa saa za Afrika Kusini na Bongo itakuwa ni saa tisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment