August 17, 2019


KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum Toto amefunguka kuwa kuongezeka kwa wachezaji katika idara ya kiungo kutamfanya azidishe juhudi ili kuilinda nafasi yake ndani ya klabu hiyo.

Feisal alikuwa katika sehemu ya kikosi cha kwanza cha Kocha Mwinyi Zahera lakini kwa sasa kocha huyo ameonekana kuwatumia zaidi Papy Tshishimbi, Balama Mapinduzi na Mohamed Banka katika eneo la kiungo.

Feisal alisema Yanga ni timu kubwa na inahitaji kuwa na wachezaji wengi wenye viwango vikubwa, baada ya ongezeko la
wachezaji anatakiwa kuongeza ubora ili pate nafasi.

“Yanga ni timu kubwa sana na inashiriki michuano mingi, lazima iwe na wachezaji wengi wenye uwezo mzuri wa kupambana na ili mimi nilinde nafasi yangu kwenye kikosi cha kwanza inabidi niongeze uwezo ndani ya Yanga,” alisema kiungo huyo.

Baadhi ya wachezaji walioongezeka katika eneo la viungo ni pamoja na Mapinduzi, Issa Bigirimana na Abdulaziz Makame ambao walisajiliwa kuongeza nguvu katika eneo la kiungo cha Yanga.

Yanga kwa sasa ipo Kilimanjaro ikijiweka sawa kwa ajili ya mchezo wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers, utakaofanyika wikiendi ya wiki ijayo Gaborone nchini Botswana.

1 COMMENTS:

  1. Sishangai yanayotokea Yanga kwenye mechi za kirafiki na za mashindano ya CAF nilishashauri huko nyuma kuwa Yanga inahitaji kuliimarisha benchi la Ufundi kuongeza ujuzi na mbinu kwani viwango vya wachezaji vinaporomoka kwa kiwango cha juu mno....uwezo wa benchi la ufundi la Yanga ni mdogo mno...na kama hatua za haraka hazitachukuliwa kuliimarisha benchi la ufundi kuna hatari sana huko mbele aibu itatokea...Mimi si tu kwamba ninatathmini mchezo wa soka kwa umahiri ninazichambua timu kutokana na mechi zinazocheza.....nilisema kuwa Yanga inahitaji kuiiga Simba kutafuta Kocha Msaidizi kutoka Ulaya au Hata Amerika Kusini au Asia au Hata Africa mwenye viwango vya FIFA....ili wachezaji waongezewe mbinu katika mashindano.....Bado Yanga wana wachezaji wazuri lakini soka wanalocheza watapata tabu wakicheza na timu zenye mbinu za kubadilisha mchezo haraka.....kwahiyo hili la kubadilisha au kuliimarisha benchi la ufundi haliepukiki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic