KOCHA msaidizi
wa timu ya Taifa ya Tanzania,‘Taifa Stars’ Seleman Matola amesema kuwa ana
imani kikosi kitakwenda kufanya kweli kwenye mchezo wao wa kufuzu Kombe la dunia dhidi ya Burundi.
Stars, itamenyana na Burundi Septemba 4 Uwanja wa Prince Louis Rwagasore, nchini
Burundi kabla ya kurudiana nao uwanja wa Taifa, Septemba 8 mwaka huu.
Matola amesema kuwa wachezaji wana morali kubwa ya
kupambana na kila mmoja anatimiza jukumu lake kwa wakati.
“Tuna kazi
ngumu ya kufanya hasa ukizingatia tutakuwa ugenini jambo ambalo limetufanya
tutumie muda mwingi kuwaandaa wachezaji wetu.
“Matumaini
ya kufanya vizuri ni makubwa, kikubwa ni sapoti ya mashabiki kuelekea kwenye
mchezo wetu kwani hesabu zetu ni kupata matokeo mazuri,” amesema.
Kilalakheri Taifa Stars, Tunawaombea Muweze Kushinda Mechi Hiyo
ReplyDeleteMuzamiru Yasini yupo vizuri zaidi hivi sasa itapendeza kama jitihada zake zikaongezewa ndimu kwa kuitwa Taifa stars .
ReplyDelete