August 4, 2019


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mashabiki msimu ujao waendelee na moto wao wa kujaza uwanja kwani ilikuwa ni tatizo kwa msimu uliopita wao kufanya hivyo.

Leo Yanga wanahitimisha wiki ya Mwananchi ambapo uwanja wa Taifa ulikuwa wazi kuanzia saa nne kamili asubuhi na kwa sasa burudani zinaendelea uwanja wa Taifa.

Zahera amesema:"Msimu uliopita kulikuwa na tatizo kidogo kwa mashabiki kujitokeza uwanjani na kuujaza uwanja ila kwa sasa mambo mengi yamebadilika hivyo wasisahau kuendeela kujitokeza uwanjani.

"Kikosi ni imara na kimeimarika zaidi ya msimu uliopita kazi ni moja tu kuendelea  kuipa sapoti timu yao," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic