August 4, 2019


PHILIPPE Coutinho, amesema kuwa hana mpango wa kutimkia Arsenal na kuiacha Barcelona kwa mkopo.

Inaelezwa kuwa Barcelona ina mpango wa kumuuza nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 ili atoe nafasi kumrejesha Neymar Jr.

Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, Barca inatarajia kumtoa kwa mkopo nyota huyo endapo kuna timu itakayokubali kutoa ada ya pauni milioni 30.

Ripoti zinaeleza kuwa Coutinho hayupo tayari kuondoka ndani ya Camp Nou kwa dili la muda na kipaumbele chake ni kubaki hapo ndani ya Barcelona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic