August 4, 2019


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa msimu ujao kikosi chake kitakuwa kwenye mwendo wa mchakamchaka kwani hakuna mchezaji atakayekuwa anakimbia.

Leo Yanga imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Kariobangi Sharks uwanja wa Taifa mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Zahera amesema ushindani msimu ujao ni mkubwa naye amejipanga kuwa na kikosi imara kitakacholeta ushindani mkubwa msimu ujao.

"Nimefurahi kuona mashabiki wengi wamejitokeza leo uwanja wa Taifa, hichi ni kitu ambacho tulikikosa msimu uliopita hivyo msimu ujao waendelee kujitokeza kwa wingi.

"Kazi yetu msimu ujao itakuwa ni kote kwani hatuna mchezaji atakayekuwa anatembea wote wanakimbia mwanzo mwisho," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic