August 16, 2019


Kikosi cha Polisi Tanzania kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Ushirika huko Moshi.

Yanga imepoteza mchezo huo ukiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mechi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Africa dhidi ya Township Rollers huko Botswana Agosti 23, 2019.

Mabao ya Polisi yamewekwa kimiani na Marcel Kaheza aliyecheka na nyavu dakika ya sita ya mchezo kwa njia ya penati.

Bao hilo lilidumu kwa dakika 45 ambazo zilimalizika kwa Polisi kuwa mbele kwa 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi tena ambapo Polisi walizidi kulisakama lango la Yanga na katika dakika ya 74, Ditram Nchimbi aliandika bao la pili.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Polisi ambao wamepanda daraja kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao walikuwa na mabao hayo mawili na Yanga wakiwa na sifuri.

7 COMMENTS:

  1. Safi kabisa!Tangu lini vyura wakaimba nje ya maji!Hiyo ndiyo inaitwa kuchezea nyumbani!Hatutashangaa AFC Leopards wakifungwa Moshi kwa sababu sio kwao!Je vyura watu walilijua hilo walipocheza na Township Dar? Mbona hawakutumia chance ya nyumbani kama walivyozitumia mechi kumi na mbili mfululizo za mwanzo za ligi kuu mwaka jana..Au wanadhani tumesahau? Ni nini kilitokea walipoanza kucheza nje ya Dar? ni kupoteza mechi na Zahera akaanza wimbo wa viporo na kubebwa! Halafu wiki nzima Saleh Jambe ni kutuandikia habari eti ohh Township watapindua matokeo kitabe Gaborone!Kwa uwezo gani? Hiyo Polisi si ndiyo kwanza wamepanda daraja?Kila la heri Yanga! Nafasi na bahati zinapokuja maishani zinapaswa kunyakuliwa na kutumiwa ipasavyo!You lost your chance!Now Good Luck!

    ReplyDelete
  2. Mbutembute kelele za kwenye magazeti tu.Hamna lolote.Huyo Molinga anarukaruka tu.

    ReplyDelete
  3. Mngetuachia tu Yanga yetu ileile mbovu jamani!

    ReplyDelete
  4. Kama unatafuta kocha mbishi, asiyetambua mahitaji ya yanga, aliyetuletea wachezaji waajabu, aliyeiuza timu kama atakavyo basi utampata Zahera. Timu haitaenda popote bali ni kubaki mahome tu.

    ReplyDelete
  5. Msimu huu wa ligi kazi ipo. Kingine imethibitika Zahera hamuwezi Matola hakuna ubishi yaani Zahera kiboko yake ni Selemani matola.

    ReplyDelete
  6. Ni mechi ya kujipima kama wanaweza kuitoa Town au kunyakuwa ubingwa. Huenda ikawa refa kama vile walivokuwa msimu iliopita. Almuradi yetu Ni macho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic