HASSAN Kabunda, kiungo
mshambuliaji wa KMC alivunja rekodi iliyowekwa na
KMC ya kutopata ushindi ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kufunga bao lake la kwanza msimu huu uwanja wa Azam Complex.
Kwenye michezo miwili
ambayo ni sawa na dakika 180, KMC haikuambulia pointi wala bao mpaka
ilipocheza na Namungo na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Hassan Kabunda amesema kuwa ushindani umekuwa mkubwa jambo
linalowafanya waimarike taratibu.
"Kwa sasa bado
ligi inaanza licha ya kushinda bado tuna kazi kubwa ya kufanya mbele huu ni
mwanzo tu mashabiki watupe sapoti," amesema.
KMC imefungwa jumla ya
mabao matatu kwenye mechi tatu ilizocheza mpaka sasa huku wao wakiwa wamefunga
bao moja pekee.
0 COMMENTS:
Post a Comment