September 27, 2019



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa uamuzi juu ya dhamana pamoja na mashitaka ambayo walifutiwa waliokuwa viongozi wa Simba wiki iliyopita. 

Hii ni baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba awali alipanga kutoa uamuzi leo Ijumaa lakini kumbe muda alipanga ulikuwa mfupi kuweza pitia uamuzi ule.

Hakimu huyo alitakiwa kutoa maamuzi kwa mara nyingine kuhusiana na kuwafutia mashitaka ya utakatishaji fedha washitakiwa wawili Evans Aveva na Godfrey Nyange ambayo yaliwapa nafasi ya kupata dhamana. 

Hata hivyo maamuzi hayo ya awali ya Hakimu Simba yalipigwa na Serikali ambapo walikata rufaa Mahakama Kuu kuomba maamuzi ambayo yalitolewa yote yaweze kutenguliwa huku upande Serikali ukiongozwa Wakili Mwandamizi Serikali, Wonkyo Saimon. 

Hakimu Simba amesema kutokana na muda kuwa muda ndiyo ameshindwa kutoa uamuzi  kama watapata dhamana na kufutiwa yale mashitaka. 

Simba aliairisha kesi hiyo mpaka Oktoba 11, mwaka huu ndipo atatoa uamuzi juu ya kesi hiyo. 

Ikumbukwe wiki iliyopita mahakama ilitoa uamuzi na kuwafutia mashitaka mawili ya utakatishaji fedha waliokuwa viongozi wa Simba lakini baada serikali ilikata rufaa juu ya maamuzi hayo.

Ikumbukwe Aveva na Kaburu washitakiwa kwa makosa tisa na mawili yakiwa ni ya utakatishaji fedha pamoja na mengine ya kughushi ambapo aliunganishwa na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zachariah Hans Poppe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic