September 30, 2019


Timu tajiri Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC juzi Jumamosi jioni ilishindwa kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Sasa imewaachia Yanga ipambane kwenye hatua inayofuata.

Ilishindwa kupindua meza kibabe mbele ya Triangle FC ya hapa baada ya kukubali kipigo kingine cha bao 1-0. Hiyo inamaanisha kwamba Azam imetolewa kwenye michuano hiyo kwa idadi ya mabao 2-0 kwani awali nyumbani ilifungwa bao 1-0.

Kupoteza nafasi hiyo kuna maanisha kwamba wachezaji wa Azam wamepoteza zaidi ya Sh.Mil 20 ambazo walikuwa wameahidiwa kama zawadi kama wangesogea kwenye hatua ya mtoano.

Katika mechi ya jana Azam ilionyesha morali ya aina yake nyuma ya mashabiki wao 48 waliosafiri kutoka Tanzania. Ilicheza soka safi na kupoteza nafasi nyingi za wazi kupitia kwa mastraika wao, Obrey Chirwa na Donald Ngoma.

Azam jana ilianzisha mziki wake wote, chini ya nahodha Bruce Kangwa lakini maji yalizidi unga, jambo ambalo linamaanisha kwamba Triangle sasa huenda wakakutana na Yanga kama maajabu ya soka yatatokea kwenye droo ya mtoano.

Kocha wa Azam, Ettiene Ndayiragije aliwapooza mastaa wake na kuwaambia kwamba ni sehemu ya kujifunza hivyo wajipange kwaajili ya Ligi Kuu Bara na michuano mingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic