BREAKING: AVEVA NA KABURU KUACHIWA KWA DHAMANA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na wenzake katika mashitaka 8 isipokuwa mawili ya utakatishaji fedha.
Kutokana na Hatua hiyo Washtakiwa Aveva na Godfrey Nyange wamepewa masharti ya dhamana kuwa na wadhamini wawili watakaosaini Bondi ya Sh30 milioni lakini masharti hayo wameshindwa kuyatimiza kutokana na madai yakuwa hawakujianda na hivyo mda wowote kuanzia kesho wanaweza kupata dhamana yao.
Hivyo Hakimu Mkazi Mkuu Thomasi Simba amesema katika mashtaka hayo mawili ya utakatishaji wa fedha ameyaondoa hivyo dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa hivyo wawe na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh30 milioni.
Kutokana na hatua hiyo washtakiwa hao wamepatiwa masharti ya dhamana kwa sababu mashitaka ya utakatishaji fedha ambayo yaliwanyima dhamana hayapo.
Daaaaaaahhh!!!!!!Dar DSM sema Dar es Salaaaaaam......!!kweli Dar sio sehemu ya kushangaa. Baada ya muda mrefu. Naamini dhamana haiwezi kukosekana. Mpira mzeee ni nouma sana. Kama kaka angu Aveva namshauri aache kabisa huko
ReplyDelete