September 29, 2019


MIONGONI mwa tatizo kubwa linaloikabili timu ya Manchester United ni pamoja na kuundwa na vijana wengi chipukizi.

United iliyo chini ya Ole Gunnar Solskjaer ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa imecheza michezo sita na ina pointi 8 imeshinda michezo miwili, imepoteza miwili na kutoa sare mbili.

Kesho itakuwa na kibarua kingine mbele ya Arsenal ambayo ipo nafasi 8 na imecheza jumla ya mechi sita na ina pointi 11 imepoteza mchezo mmoja pekee na ina sare mbili na imeshinda mechi tatu.

Mpaka sasa, Solskjaer anawaamini vijana ambao ni Darren James, Andreas Pereira, Marcus Rashford.

Pia kwa sasa kukosekana kwa Paul Pogba kunaigharimu timu kwani Mc Tominay amekuwa tegemeo katika kuchezesha na Nemanja Matic ameshuka kiwango benchi linamhusu.

Ikumbukwe, Matic, Ashley Young na Juan Mata umri umewatupa mkono na kusepa kwa Lukaku kwenda Inter Milan na Sanchez kwa mkopo ni tatizo.


Solskjaer amesema kuwa ana imani na kikosi chake taratibu kinaaimarika na kitakuwa na matokeo chanya mbeleni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic