Rekodi zinaonyesha kwamba, Mbwana Samatta ameshacheza jumla ya mechi 209 kutoka mwaka 2010.
Samatta amefunga jumla ya mabao 109 kwa ngazi ya klabu pekee achana na yale aliyofunga akiwa Mbagala Market ambayo kwa sasa ni African Lyon.
Mkononi ana rekodi ya kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, ubingwa wa Super Cup, Kushiriki Kombe la Dunia la klabu akiwa na TP Mazembe pamoja na mshikaji wake Thomas Ulimwengu.
Pia ana tuzo ya mchezaji Bora wa Afrika Kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za ndani na alizama mazima kwenye kikosi Bora cha Afrika mwaka 2015.
2016 alitua Ubelgiji ndani ya KRC Genk na hakutamba ndani ya misimu miwili ya mwanzo ila msimu uliopita mambo yalianza kunyooka kwake.
Ameipa ubingwa wa Ligi Kuu ya Ubelgiji na Kombe la Super huku akiibuka kinara wa utupiaji kwa wachezaji wanaotokea Afrika na kupewa tuzo ya Ebony Shoe kwa kupachika mabao 23.
Pia ni Mtanzania wa Kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufanikiwa kufunga bao.
0 COMMENTS:
Post a Comment