September 1, 2019



Matokeo ya Manchester United kwa sasa michezo minne ya EPL yapo namna baada ya kucheza michezo minne na kukusanya pointi tano pekee.

 Manchester United ilianza kusinda kwa mabao 4-0  dhidi Chelsea uwanja Old Trafford.

Wapachika mabao ni Marcus Rashford dk ya 18 kwa penalti na 67 Anthony Martial dk ya 65 na Daniel James dk ya 81.

Pia ililazimisha sare mbele ya Wolves 1-1 United, ilikuwa Uwanja wa Molineux.

Bao la Wolves lilifungwa Ruben Neves dk ya 55 na United lilifungwa na Anthony Martial dk ya 27.

Ilipata kichapo mbele ya Crastal Palace kwa kukubali kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa Old Trafford wapachika mabao Kwa Crystal Palace ni Jordan Ayew dk ya 32 na Patrick van Aanholt dk ya 90+3 huku kwa United akiwa ni Daniel James dk ya 89.

Kwenye mchezo wa jana dhidi ya Southampton ililazimisha sare ya kufungana bao  1-1. Kwenye mchezo huo kadi nyekundu ilionyeshwa kwa Kevin Danso wa Southampton dk ya 73 na bao la Southampton limefungwa na Jannik Vestergaard dk 58 na Kwa United Daniel James dk ya 10.

Paul Pogba na Marcus Rashford wamekosa penalti kwenye michezo miwili tofauti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic