IMEELEZWA kuwa nyota wa Liverpool, Virgil Van Dijk ambaye amebeba tuzo kubwa ya kuwa Mchezaji Bora wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) aliwaacha kwa mbali wapinzani wake wa karibu aliokuwa akipambana nao.
Kwenye usiku wa tuzo za UEFA, Dijk alisepa na tuzo mbili ambapo alianza kutwaa ya beki bora kaba ya kusepa na ile iliyokuwa ikitazamwa na wengi ya Mchezaji Bora wa Ulaya.
Kipa wake Allison alisepa na Tuzo ya Kipa Bora wa UEFA huku wakongwe katika gemu, Lionel Messi na Cristiano Ronado wakiachwa mbali kwa kura.
Dijk alikuwa msaada mkubwa kwa kuiwezesha Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita inaelezwa kuwa alipata kura mara tatu zaidi ya washindani wake.
Kwa tuzo hiyo anakuwa ni Mholanzi wa kwanza kushinda tuzo hiyo kubwa kwa wachezaji wa kiume.
Ni Haki Yake Kupata Tuzo Hiyo, Hongera Yake
ReplyDelete