KIONGOZI SIMBA AWAKATAA YANGA, ASEMA KWA ZESCO WANAENDA KUKAMILISHA RATIBA TU
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Hassan Dalali, ameibuka na kusema kuwa Yanga walijiharibia wenyewe katika mechi dhidi ya Zesco United ya Zambia katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Dalali ameeleza kuwa Yanga walipswa kutumia faida ya uwanja wake wa nyumbani walipocheza jijini Dar es Salaam lakini badala yake haikuwa hivyo.
Katika mechi hiyo ambayo mbali na Yanga kulazimishwa sare ya 1-1, vilevile iliruhusu kutawaliwa kimchezo na miamba hao wa Zambia.
Aidha, Dalali ameinyima nafasi Yanga ya kupata matokeo mbele ya Zesco itakayokuwa kwao Ndola, Zambia katika mechi ya marudiano Septemba 28 2019.
"Mimi siwapi nafasi Yanga kwenye mechi ya marudiano.
"Nasema hivyo sababu hawakutumia vizuri nafasi waliyoipata wakiwa Dar es Salaam, kule wanaenda kukamilisha ratiba pekee.'
kwani wao mikia na songo walchezea wapi? mbona hawajatumia fursa ya uwanja wa nyumban? uzur wa yanga wanapambana popote hawajal nyumban wala ugenn, na ndo mana mwaka jana walpgwa nyng ugenn kutegemea sana nyumban huo udhaifu mbona mamelod amempga mtu 5 kwao mpra cku hz unapgwa kokote hata kama ukawa kwako kwan rolaz aliagia wap mashndano tz au botswana.?
ReplyDeletemchezo hauhitaji ushabiki sana kuliko uhalisia acha hasira kijana, angalia hali ya timu iko vipi kwa sasa, usikubali kutawaliwa na mifano na ukakubali kutawaliwa na ushabiki utakuwa mtumwa
DeleteZesco 2 Yanga 0 mechi ya marudiano Ndola September 28, 2019
ReplyDelete