ALIYETOKEA TIMU YA VIJANA YAMKUTA SIMBA
Kiungo mwenye zali la kupendwa na mashabiki wa Simba, Said Ndemla anadodea benchi. Amekata tamaa ya kuvaa uzi wa kikosi cha kwanza msimu huu.
Rekodi zinaonyesha kuwa Ndemla mara ya mwisho kupata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza ilikuwa Mei 8 katika mchezo dhidi ya Coastal Union msimu uliopita.
Ambapo tangu apate nafasi amekosa michezo saba ya mwisho ya ligi msimu ulioisha pamoja na miwili ya mwanzo msimu huu, akikosa hata nafasi ya kuwa mchezaji wa akiba. Jumla anakuwa amekosa michezo tisa ambazo ni sawa na dakika 810 za uwanjani.
Ukiachana na ligi kuu, mara ya mwisho Ndemla kupata nafasi ya kucheza ilikuwa katika michezo miwili ule dhidi ya Sevilla na Gwambina FC ambapo alifunga bao la kusawazisha.
Hali inazidi kuwa ngumu kwa mchezaji huyo kutokana na uwepo wa viungo wengine kama Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Sharaff Shiboub, Mzamiru Yassin, Clatous Chama, Gerson Fraga na Francis Kahata ambao wote wameshapata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha Simba.
“Nafasi yangu naiona finyu sana msimu huu haswa baada ya timu kuondolewa kwenye mashindano ya kimataifa, kwa vile kule wangecheza wengine na sisi tungetamba huku, lakini mambo yamegeuka,” aliongeza mchezaji huyo aliyewaringia Yanga na kusaini Simba.
Muandikaji umeyavulia nguo ya Ndemla. Mwalimu ana hesabu na mipango yake na kila akifanyacho Kwanza maslaha ya timu na vilevile masilaha ya kila mchezaji yakiheshimiwa Mia Kwa mia
ReplyDeleteHii habar ya ndemla mbon mnaipenda sana h n zaid ya mara 4 sasa hukitok huk mna amia kwa gazet lenu la sport xtra bado mnaandik alichosem muda sana...unafikir hao wanaochez watakua kwa kiwango hicho hicho msim mzima...ndeml atachez sana t
ReplyDeleteAliwalingia au hakuwa na nia naye wenyewe, we mwandishi unamatatizo
ReplyDeleteWaseche nyie..
ReplyDeleteKilichoandikwa wala hakina ubishi mie nashangaa nyie mipovu inawatoka tu,kama mchezaji hapewi nafasi ya kucheza na timu yake,waandish wa habar ni jukumu lao kuwahabarish watu,na asipocheza akae akijua kiwango chake kitashuka tu,hapa ndio mchezaji unapata funzo kama kuna timu inakutaka na imekuhakikishia kupata nafas ya kucheza ni bora ufanye kwenda huko na sio kwenda sehem ambayo unajua kabisa uwezekan wa kucheza ni mdogo
ReplyDeletekwa hyo unataka apewe nafasi ya kucheza ili akidhi mahitaji yake timu idode wewe msimu ndo hapatyi maana timu zinashuka sana pengne simba iwe inafunga mapema yeye anaingia kukamilisha ratiba
DeleteHuyu muandishi. Yamemuumiza yeye kuliko yeye mwenyewe Ndemle. Wacha Futuna yako
ReplyDeleteMie sioni Tatizo la kuendelea kucheza Simba hata kama anakaa benchi Kwani hapa muhimu kwake kwanza ni pesa ya usajili na maslahi kama mshahara anao pata kuliko angechezea klabu nyingine ambazo haziwezi kumpatia maslahi anayopata Kwa sasa Simba.
ReplyDeleteKila mchezaji ana mahesabu yake ktk maisha na kama
hataki kuchezea klabu nyingine Tanzania zaidi ya Simba?Kila binadamu ana malengo yake binafsi ambayo tulio nje ya familia yake hatupaswi kujua wala kuhoji.
Ligi kuu ndio kwanza mechi ya pili na mwezi wa kumi unakaribia huku ratiba ya kila timu kucheza mechi 38 kabla ya mwezi wa sita mwaka 2020, Azam kombe la shirikisho bado, Mapinduzi cup bado. Simba wanahitaji kila mchezaji waliyekuwa nae Ndemla akiwemo. Na haya maneno ya mchezaji fulani ni zaidi ya mwengine ni ya kufitinisha tu. Wachezaji hawashindani wao kwa wao. Mafanikio ya timu ndio yanayobeba cv zao.
ReplyDelete