September 30, 2019


Mchecheto mkubwa uliowakumba mashabiki wa Yanga baada ya kuumia kwa kiungo wao mshambuliaji wanayempenda, Mapinduzi Balama sasa umefutika.

Hiyo ni baada ya Balama ambaye aliumia kifundo cha mguu katika mchezo wa kimataifa dhidi ya Zesco United ulichezwa jijini Dar es Salaam kusema kuwa anaendelea vizuri.

Balama amesema kuwa tayari ameshaanza mazoezi mepesi hivyo wachezaji wenzake watakaporudi kutoka nchini Zambia ataungana nao tayari kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania.

“Naendelea vizuri sana na nimatumaini yangu kuwa katika mchezo ujao wa ligi kuu nitakuwa sawa. “Kwa hiyo wapenzi na mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi naamini nitakuwa fiti,” alisema Balama.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic