September 15, 2019


Kocha wa viungo wa Simba, Adel Zrane ameweka wazi kuwa hakuna ruhusa kwa wachezaji wa Simba kwenda gym bila kupewa program maalumu ya kufanya na atakayekiuka adhabu itamuhusu.

Zrane alisema kuwa kumekuwa na tabia ya ajabu kwa baadhi ya wachezaji wa Simba kukimbilia kwenda gym kufanya mazoezi bila kuwa na program maalum.

“Wachezaji wote ni lazima wawe na program maalum ya kufanya mazoezi sio kwa kuwa umejisikia kwenda gym basi unakwenda, kwa nitakayemgundua hana ruhusa nitakula naye sahani moja,” alisikika kocha huyo akiwaambia wachezaji wake.

Alipozungumza na Championi, Zrane alisema: “Siwakatazi wachezaji kwenda gym ila ninachowataka ni kwamba wawe wanatoa taarifa kisha ninawapa program maalumu ambayo itawasaidia waweze kujijenga na kwenda na mfumo wa Simba.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic