September 15, 2019


Mkali wa Afro Pop kutoka Nigeria, Burna Boy amefanya tukio la ajabu mara baada ya kumtoa nje shabiki aliyekuwa hashangilii shoo yake aliyofanya juzi huko Atlanta Georgia, Marekani.

Burna Boy alifanya tukio hilo akiwa katikati ya shoo ambapo alisimamisha muziki na kumpa fedha shabiki huyo wa kiume ambaye alionekana kukosa furaha muda mwingi na kumuamuru atoke nje ya ukumbi huo.

Katika moja ya video zinazosambaa mtandaoni, zinamuonyesha mkali huyo anayetamba na Ngoma ya Gum Body, inamuonyesha Burna akisimamisha shoo na kumfuata jamaa na kumpa fedha kisha akatoa ishara ya kumwambia atoke ukumbini hapo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic