KOCHA SIMBA AMPA UFUNGAJI BORA MEDDIE KAGERE
Licha ya straika wa Simba, Meddie Kagere kuwa ndiye kinara kwenye orodha ya wafungaji akiwa na mabao matatu, kocha wake Mbelgiji Patrick Aussems, amesema kuwa bado anataka kuona straika huyo anafunga mabao mengi zaidi kwani anapata nafasi za kufunga nyingi.
Kocha huyo amesema kuwa Kagere sambamba na washambuliaji wake wengine, wanatakiwa kuongeza kasi ya kufunga kutokana na nafasi nyingi wanazopata katika kila mechi zao.
Kagere ndiye anaongoza kimabao akiwa sawa na Lucas Kikoti wa Namungo baada ya wote kufunga mabao matatu kwenye mechi mbili walizocheza za ligi hadi sasa.
Mbelgiji huyo ameliambia Championi Jumatano, kuwa anamtaka Kagere na washambuliaji wake wengine kuongeza kasi yao ya kufunga kwani wanapata nafasi nyingi za kufunga lakini wanakosa umakini.
“Nimeridhishwa na pafomansi ya timu hadi sasa baada ya mechi zetu mbili tulizocheza. Nimeangalia kwenye eneo la kiungo na ulinzi nimeona hakuna tatizo hata kidogo lakini tunakosa umakini hasa kwenye eneo la tatu la umaliziaji.
“Kwenye hizo mechi mbili tulizocheza kuna nafasi nyingi sana tunapata lakini tunakosa kufunga, ni lazima tufanyie kitu ili tukipata nafasi basi tuitumie vizuri na kushinda mabao mengi zaidi ya haya ambayo tumefunga kwenye mechi hizi,” alisema Aussems.
0 COMMENTS:
Post a Comment