September 20, 2019


Mwanamuziki  Lawrence Marima maarufu kama Marlaw ambaye aliwahi kutamba na wimbo wa ‘Bembeleza’, jana Septemba 19 2019,  amefika studio za +255 Global Radio zilizopo Jengo la Global Group Sinza Mori jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kutambulisha nyimbo zake mpya za ‘Baraka’ na ‘Taa’ ambazo zimekuja miaka tisa baada ya ukimya wake kwenye muziki.

Marlaw alipiga stori na watangazaji wa Bongo255 na kufunguka vitu vingi ikiwemo nafasi yake kwenye muziki ambayo anahisi bado ipo kutokana na vitu vizuri alivyoviandaa kwa ajili ya mashabiki wengi wanaomdai kazi mpya kila wanapomuona.

Marlaw anasema sababu kubwa iliyomfanya awe kimya kwa muda mrefu ni kutaka kujiboresha kwa kila kitu ikiwemo ubunifu, ubora, uimara na maisha kwa ujumla.

Marlaw amesema licha ya kujiandaa kuja upya kwenye muziki, familia yake na Besta ambayo imebarikiwa watoto watan,  moja ya vitu vilivyomfanya awe kimya kwa miaka mingi.

Kuhusu mke wake, Marlaw amesema Besta yupo ‘fiti’ na mipango ya kurudi kwenye muziki ipo kwani kazi walizofanya ni nyingi na muda wowote zinaweza kuachiwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic