September 17, 2019



MAKOCHA wa JKT Tanzania na Singida United,  wamegeuka mbongo kwa kupoteza michezo miwili mfululizo kwenye ligi kuu ambazo ni sawa dakika 180.

JKT Tanzania iliyo chini ya Abdallah Mohamed ‘Bares’ ilipoteza mchezo wa kwanza mbele ya Simba kwa kufungwa mabao 3-1 uwanja wa Uhuru pia ikapoteza mchezo wa pili uwanja wa Isahmuyo dhidi ya Lipuli na Singida United ilipoteza mchezo wa kwanza mbele ya Mwadui kwa kufungwa bao 1-0 na  imefungwa mabao 2-0 na Namungo.

Kocha wa JKT Tanzania, Bares, amesema kuwa wamekuwa wakitengeneza nafasi nyingi ila wanashindwa kuzimalizia kutokana na ubutu wa safu yake ya ushambuliaji.

“Kuna tatizo kwenye safu ya ushambuliaji ila kwa kuwa bado ligi ndio inaanza tuna nafasi ya kufanya vizuri michezo yetu ya mbele,” amesema Bares.

Felix Minziro, Kocha wa Singida United amesema kuwa ugumu upo kwenye umaliziaji kutokana na kuwa na wachezaji wengi wapya taratibu kikosi kinaimarika.

“Kikosi ni kipya kina wachezaji wengi ambao hawajazoeana taratibu wanazidi kuimarika na watakuwa kwenye ubora wao huo ubutu utamalizika,” amesema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic