September 17, 2019


Baada ya Yanga kutoka sare ya bao 1-1 na Zesco United Jumamosi iliyopita, mashabiki wa timu hiyo wanatakiwa wasikate tamaa kutokana na rekodi nzuri waliyonayo pindi wanapocheza mechi za ugenini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imeanza kwa kupata sare hiyo ikiwa nyumbani katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Marudiano yatakuwa ni Septemba 27 ‘machinjioni’ kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa, Zambia.

Yanga katika michezo kumi ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyocheza ugenini kuanzia 2014 imeshinda mitano, sare tatu huku ikiwa imepoteza miwili pekee.

Katika michezo hiyo, ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Komorozine ya Comoro mwaka 2014, bao 1-0 dhidi ya De Joachim ya Mauritius 2016, mabao 2-1 dhidi ya APR ya Rwanda 2016, mabao 5-1 dhidi ya Ngaya Club ya Comoro 2017 na bao 1-0 dhidi ya Township Rollers ya Botswana mwaka huu.

Mechi ambazo ilitoa sare ni 0-0 dhidi ya Zanaco ya Zambia 2017, 1-1 dhidi ya St Louis ya Visiwa vya Shelisheli 2018 na 0-0 dhidi ya Township Rollers ya Botswana 2018, huku ikipoteza mara mbili dhidi ya Al Ahly Misri mechi ya kwanza 1-0 mwaka 2014 na nyingine 2-1 mwaka 2016.

Lakini Zesco nao wanajivunia rekodi yao bora nyumbani kwenye Ligi ya Mabingwa, hatua ambayo inafanya mchezo huo wa Septemba 27 utarajiwe kuwa mkali na wa kusisimua.

Wakiwa nyumbani, Zesco wana rekodi nzuri ya kutokupoteza mchezo kirahisi kwani kwenye michezo kumi wakiwa nyumbani, wamepoteza mchezo mmoja tu baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast 2018.

Katika michezo kumi ya nyumbani hivi karibuni, Zesco wameshinda michezo saba nyumbani dhidi ya Al Ahly ya Misri, Asec Mimosas ya Ivory Coast, Mamelod ya Afrika Kusini, JKU ya Zanzibar, AS Sonidep ya Nigeria, Horoya ya Guinea na Green Mamba ya Zimbabwe huku wakitoka sare michezo miwili dhidi ya TP Mazembe na Etoil Du Sahel na kupoteza mchezo huo mmoja.

Yanga ili ifanikiwe kusonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, inahitaji kupata ushindi wa aina yoyote au sare ya mabao kuanzia 2-2.

3 COMMENTS:

  1. Mmmh mambo ya takwimu hayo. Ingawa kuangalia aina ya timu zilizofungwa na Zesco ikiwa nyumbani ni vitu viwili tofauti na timu zilizofungwa na Yanga ikiwa ugenini. Ngoja tusubiri ikiwa Yanga itakuwa timu ya pili kushida au timu ta nane kufungwa na Zesco!!!!

    Kuna wakati nashawishika kuamini kwamba namba zinadanganya!!!!

    ReplyDelete
  2. Hizi takwimu nyingine Ni kichekesho.

    ReplyDelete
  3. Acha kuwa mnaandika kishabiki na vitu mnavyotamani vitokee..Mpira sio wishful game.!kwa kuwa mwaka juzi na mwaka huu Yanga ilifanya vema dhidi ya Township Rollers hadi kwao Botswana imekuwa ndio wimbo wa rekodi inaibeba Yanga..Ndiyo ilingia makundi ikapangwa na US Algiers, Gor Mahia na Timu ya Rwanda nadhani ni Rayon Sport.Je na hapo rekodi iliwabeba? Labda umesahau tukumbushane...Waalgeria na Wakenya waliifunga Yanga nyumbani na ugenini..Kigali Yanga ilifungwa...Sasa ni rekodi gani mwandishi unafikiria wewe? Wiki iliyopita nzima tulikuwa ni kuandikiwa jinsi Zesco itafungwa!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic