PEP Guardiola, Meneja wa Manchester City amesema kuwa wachambuzi wa masuala ya mpira hawapaswi kuwa na hofu juu ya uwezo wa wachezaji wake ndani ya Ligi Kuu England lazima atawashangaza kama alivyofanya msimu uliopita na kutwaa ubingwa.
Man City kwa sasa ni timu ya kwanza kushusha kichapo cha mabao mengi ndani ya ligi ambapo iliwatandika Watford mabao 8-0 hivi karibuni na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kushinda mabao matano ya haraka ndani ya dakika dakika 18 za mwanzo.
Awali rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Blacburn Rovers iliyofunga mabao matano ndani ya dakika 24 dhidi ya Sheffield Wednesday mwaka 1997.
"Baada ya kupoteza mbele ya Norwich nilisema kwamba kama mnatutilia shaka ni tatizo lenu siyo langu, inaweza ikatokea unapoteza mchezo mmoja lakini kama unachambua kile ambacho vijana wangu wamefanya kwa misimu miwili iliyopita hilo ni tatizo kwenu.
"Labda mnaamini kwamba timu yangu haiwezi kupoteza, hilo linawezekana hawa ni binadamu na hufanya makosa," amesema.
Kesho City itakuwa na kibarua cha kumenyana na timu ya Everton na safari hii itakuwa ugenini.








0 COMMENTS:
Post a Comment