DALALI AWATAKA CHILUNDA NA NADDO
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Hassan Dalali, amemtaka Kocha Mkuu wa Azam FC, Mrundi, Etienne Ndayiragije, kuhakikisha anaawanzisha wachezaji Shaaban Chilunda na Idd Seleman 'Naddo' katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Triangle FC ili kupindua matokeo.
Azam itakuwa na kibarua kizito cha mkondo wa pili wa mashindano hayo kitakachopigwa Jumapili ya Septemba 29 kwenye uwanja wa Gibbo uliopo mjini Triangle, Zimbambwe.
Dalali ameeleza kuwa Naddo na Chilunda ni wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Azam ambao kama wakianza, wanaweza kufanya chochote ndani ya dakika 90 ambazo anaamini zitakuwa ngumu sababu ya kila timu kutaka kusonga mbele.
Amewasifia akieleza uwepo wao katika timu ya taifa hawana sababu ya kuachwa au kuanzia benchi, kutokana na njaa yao ya kulitaka lango la wapinzani wanapokuwa kibaruani kuipigania timu yao.
"Kiuhalisia mechi itakuwa ngumu kutokana na Triangle nao watakuwa wanahitaji kupata matokeo, ni vema Ndayiragije akawaanzisha Naddo na Chilunda ambao mimi nawaamini wanaweza kuipa matokeo Azam.
"Nawafahamu vizuri wakiwa uwanjani wanakuwa na njaa ya kucheka na nyavu na uzuri zaidi wapo timu ya taifa, sasa kuna haja gani ya kutokuanza?
"Kama Azam wanataka kupindua matokeo wawatumie vizuri wale vijana pale mbele na bila shaka watafanya kile ambacho mimi nakitegemea," alisema Dalali.
Kwa upande mwingine, Dalali amewataka Azam kucheza kwa tahadhari kubwa na kuboresha mapungufu yote yaliyojitokeza katika mechi ya mkondo wa kwanza ili waweze kufanya vema.
Ikumbukwe baada ya Azam kupoteza kwa bao 1-0 katika mechi ya awali jijini Dar es Salaam, ili iweze kusonga mbele, inapaswa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.







Naddo na Chilunda walishindwa kuipa matokeo Stars dhidi ya timu ya kawaida kabisa, Sudan watawaweza Triangle kwao? Ni wachezaji wa kawaida sana.
ReplyDeleteHuwez kujaji kwa game moja walio mzunguka star na azam n tofaut kumbuk hilo mpira n mchezo wa mbin na kutumia nafas haijalish kiwang ulicho nacho
ReplyDelete