MKUDE ATIBUA MIPANGO YA MBELGIJI SIMBA
Kiungo Jonas Mkude unaambiwa amemtibulia mipango kocha mkuu wa kikosi cha Simba, Patrick Aussems kiasi kwamba bosi huyo ameamua kubadilisha kila kitu katika programu za mazoezi yake.
Kocha huyo raia wa Ubelgiji amelazimika kubadili kila kitu kwenye programu zake za mazoezi kutokana na kumkosa Mkude sambamba na wachezaji wengine saba ambao wameondoka kwenda timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiandaa na mechi dhidi ya Sudan.
Mkude ni miongoni mwa wachezaji ambao wana uhakika wa kuanza kwenye kikosi cha Simba ambaye ameenda Stars, wachezaji wengine ni Erasto Nyoni, Miraji Athuman ‘Sheva’, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Gadiel Michael na Haruna Shamte.
Aussems alisema, tangu waanze proramu wiki hii anashindwa kufundisha mbinu nyingi kutokana na uchache wa wachezaji wake ambapo nane wameenda Stars.
“Unaona hapa nina wachezaji 16 tu, wengine ni majeruhi na wengine wameenda Stars. Walioenda Stars ni wengi kiasi kwamba hata nashindwa kufundisha mbinu zangu zote,” alisema Aussems.
0 COMMENTS:
Post a Comment