KUELEKEA
kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kesho uwanja wa Isahmuyo kati
ya JKT Tanzania na Mtibwa Sugar, makocha wote wawili wameanza kutumiana tambo kabla ya kukutana uwanjani.
JKT Tanzania
na Mtibwa Sugar zote zitakutana zikiwa na machungu ya kupoteza pointi sita za
mwanzo kwenye ligi ambapo Mtibwa Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu Zuber Katwila
ilipoteza mchezo wa kwanza uwanja wa Samora kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya
Lipuli na mchezo wa pili mbele ya Simba uwanja wa Uhuru kwa kufungwa mabao 2-1.
JKT Tanzania chini ya Kocha Mkuu, Abdallah Mohamed ‘Bares’ ilipoteza mchezo wa kwanza
mbele ya Simba kwa kufungwa mabao 3-1 na mchezo wa pili ilipoteza ikiwa nyumbani
kwa kufungwa bao 1-0 na Lipuli sasa itawakaribisha Mtibwa Sugar.
Bares
amesema : ”Tumegundua makosa yetu kwenye michezo iliyopita kwa sasa
tunayafanyia kazi mapungufu yetu ili kufanya vema, tunawaomba mashabiki watupe
sapoti tunahitaji ushindi hakuna jambo lingine.
Katwila
amesema: “Matokeo chanya ndio kitu ambacho tunahitaji, kushindwa kwenye
michezo ya nyuuma haina maana kwamba hatuwezi, uwezo upo na makubwa yanakuja,
tunahitaji ushindi na inawezekana kwani wachezaji wana morali kubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment