MOLINGA AAHIDIWA MILIONI MBILI AKITUPIA BAO KAMBANI
Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera ametenga kitita cha milioni mbili kwa ajili ya kununua mabao ya straika wake David Molinga ‘Falcao’ raia wa DR Congo katika Ligi Kuu Bara.
Zahera ametenga kitita hicho ikiwa ni baada ya straika wake huyo kuanza kuonyesha cheche kwa kufunga mabao matatu kwenye mechi zao mbili zilizopita za kirafiki.
Molinga alifunga mabao hayo kwenye mechi za timu hiyo dhidi ya Pamba SC na Toto African wakati walipokuwa Mwanza wiki chache zilizopita.
Zahera amesema kwamba atatoa kiasi hicho cha milioni 2,293,230 (sawa na dola 1,000) endapo kama itatokea straika wake huyo atashindwa kufunga mabao 15 au zaidi kwenye ligi kuu. “Mimi ninasema nitatoa kiasi cha dola 1,000 kama itatokea Molinga hatafunga mabao 15 kwenye ligi kuu.
Ninamjua ana uwezo mkubwa wa kufunga tofauti na watu ambavyo wanamchukulia,” alisema Zahera ambaye ameuweka kando uraia wa DR Congo na kuchukua wa Ufaransa.
“Hapa kwenye kikosi changu tatizo lililopo ni washambuliaji tu kushindwa kufunga mabao. Sisi kwenye mechi moja tunaweza kupata hadi nafasi sita lakini tukafunga mabao machache huku nyingi tukikosa.
“Yaani hatuna shida kabisa kwenye kutengeneza pasi za mabao ila tatizo ni kufunga lakini muda si mrefu nitatengeneza mbinu ambayo itafanya tufunge katika kila nafasi ambayo tunaipata,” alisema Zahera ambaye ana mtihani mkubwa wa kuivusha Yanga kimataifa ili kurejesha imani ya kikosi chake kwa mashabiki
HUELEWEKI,UTATOA KUMPA NANI ENDAPO ATASHINDWA KUFIKISHA MABAO 15 YA LIGI KUU??FUNGUKA ILI KESHO ISIJE KUA TAABU.
ReplyDeleteWewe ndie huleweki usiyefatilia. Zahera alitoa ahadi hiyo kuwaahidi waandishi wa habari waliokuwa wakimuhoji kuhusu uwezo wa Molinga na akawaambia, akishindwa atawapa milioni 2.
ReplyDeleteEnter your comment...ahsante kwa mrejesho,barikiwa sana
ReplyDeleteMh
ReplyDelete