Na George Mganga
Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema anahitaji mchango kutoka kwa wadau haswa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo pamoja na Simba ili kulipa deni analodaiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, baada ya kufanyiwa operesheni ndogo tumboni.
Akilimali alifanyiwa operesheni hiyo kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari alionao kwa muda mrefu mpaka kupelekea kufanyiwa matibabu lakini hajafanikiwa kulipa deni ambalo ni shilingi za kitanzania 369,000 tu.
Akilimali amesema amekuwa na ratiba ya kwenda hosptalini Muhimbili kwa ajili ya kucheki afya kutokana na maagizo aliyopewa na Daktari wake lakini akieleza gharama za safari na deni alinalo zimekuwa kubwa.
"Hali yangu si mbaya kwa sasa, naendelea vizuri lakini nadaiwa shilingi 369,000 na mpaka sasa sijalipa chochote, naomba kama wadau wataguswa na kuumwa kwangu wanisaidie walau hata kidogo.
"Inabidi nianze kulipa walau kidogokidogo maana sasa nikienda hospitali kwa ratiba niliyopewa na Daktari nitakuwa sifanyiwi huduma maana sijalipa chochote, hata wao wamenitaka nilipe la sivyo sitahudumiwa," alisema Akilimali.
Akilimali amesema kama kuna mtu ataguswa kwa namna moja ama nyingine na namna hali yake ilivyo, anaweza kumchangia chochote kupitia namba yake ya simu ambayo ni 0658668819 na jina ni IBRAHIM OMARY AKILIMALI.
Aidha, Akilimali amewashukuru baadhi ya watu walioguswa na suala lake ambao wamekuwa wakienda nyumbani anapoishi kumpa pole.
0 COMMENTS:
Post a Comment