September 1, 2019


Baba mzazi wa mshambuliaji, Mbwana Samatta, Mzee Ally Samatta amefichua kuwa hakushangazwa na hatua ya Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) kuipanga Genk anayochezea mtoto wake huyo kundi mmoja na Liverpool ya England kwa kuwa ilikuwa ndoto yake.

Samatta anayecheza katika Klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji atakuwa na nafasi ya kucheza dhidi ya Liverpool katika Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi, ikipangwa Kundi E na timu ya Napoli na Reb Bull.

Mzee Samatta alisema kuwa kwa upande wake hakushangzwa na hatua hiyo kwa kuwa tayari Samatta alishamueleza ndoto yake ya kutaka kucheza dhidi ya klabu ya Uingereza katika michuano hiyo.

“Unajua mimi wala sijashangaa kuona Genk wamepangwa kundi moja na Liverpool, Napoli na wale Red Bull kwa sababu siku moja kabla Samatta alinipigia na kunieleza ndoto yake kwamba anatamani kuona wanapangwa na klabu za Uingereza na kweli ameipata hiyo Liverpool.

“Sasa nadhani kazi ipo kwake ya kwenda kuonyesha ubora kwa kuwa anakwenda kukutana na beki bora, Virgil van Dijk na yule kipa wao, Alisson Becker, akiweza kuwafunga hao basi atakuwa ameshafungua milango mingine kwa timu za Uingereza na kwa kuwa anafanya mazoezi katika milima ya Ubelgiji hilo naamini litawezekana,” alisema Mzee Samatta.

SCHALKE O4 WAMGEUKIA SAMATTA

Wakati Samatta akipangwa kupambana na Liver, huko Ulaya vyombo mbalimbali vya habari nchini Ujerumani ikiwemo Sky Sport.de zimeeleza kuwa kocha wa Klabu ya Schalke O4, David Wagner anataka kumsajili Samatta kwenye kikosi chake ili kwenda kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji.

Schalke wamefikia uamuzi huo baada ya kufeli dili la kumvuta mshambuliaji wa AC Milan, Andrea Silva ambapo uongozi wa klabu hiyo umegoma kumuuza kwa kipindi hiki.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic