Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini katika
klabu ya Simba, Hamis Kilomoni, amesema kikosi cha timu yao bado ni cha kawaida
kutokana na namna kilivyocheza mechi za mwanzo katika Ligi Kuu Bara msimu huu.
Mpaka sasa Simba imeshacheza jumla ya michezo miwili ya ligi
ambayo ni dhidi ya JKT Tanzania ikishinda 3-1, na dhidi ya Mtibwa Sugar ambao
iliibuka pia na ushindi wa mabao 2-1.
Kilomoni ambaye amekuwa akivutana na uongozi wa Simba
haswa Mwenyekiti wa Bodi wa Wakurugenzi, Mohammed Dewji 'Mo' kuhusiana na suala
la uwekezaji ndani ya klabu, ameeleza timu hiyo inapaswa kufanya usajili haraka
ili ifanye vizuri.
Kilomoni
amefunguka akieleza katika nafasi ya ushambuliaji timu imekuwa haieleweki
ikikosa muunganiko mzuri kwa wachezaji kitu ambacho kinapelekea umaliziaji kuwa
butu.
Ameongeza kwa kusema Simba ya msimu uliopita na sasa ni
vitu viwili tofauti, akisema hii haina mtu kama Emmanuel Okwi ambaye alikuwa na
mchango wake mkubwa haswa kwenye mechi za kimataifa.
"Kwakweli timu yetu kwa sasa ni ya kawaida licha ya
kushinda mechi zake mbili za mwanzo.
"Katika safu ya ushambuliaji ina tatizo kubwa ambalo
linapelekea tukose nafasi nyingi za wazi, hii inaweza ikaja ikatugharimu zaidi
siku za usoni maana kuna timu nyingi kwenye ligi.
"Kuondoka kwa Okwi katika namna moja ama nyingine
inaweza ikawa imeleta madhaifu kadhaa kutokana na mchango wake aliokuwa
anuonesha haswa kwenye mechi za kimataifa.
"Ni vema uongozi ukafanya usajili wa mchezaji
mwingine haraka ili tupate mtu mzuri atakayesaidiana na Kagere ambaye ndiye
amekuwa mhimili mkubwa kwenye safu hiyo hivi sasa," alisema Kilomoni.
Brother kwa weled wako luendelea kuandika habar za Kilomon ambazo hazina tija kwa soka letu unajivunjia heshma mwenyewe simama kwenye weled wako tunaoujua
ReplyDeleteHana weledi wowote.Acha kumpaka huyo.Ukiwa huna taaluma ya uandishi wa habari na kuandika kwa mazoea unategemea nini?
ReplyDeleteTuishapigwa hamsa 5 na Yanga huyo akiwa ndio alikuwa centre half.asijitoe ufahamu bado tunakumbuka
ReplyDelete