September 15, 2019


John Bocco ambaye ni nahodha wa Simba ametamba watachukua ubingwa wa ligi kuu na ule wa michuano wanayoshiriki ili kujipoza machungu ya kutolewa mapema kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bocco ambaye hajacheza mechi mbili za ligi kuu ambazo Simba wameshacheza mpaka sasa kutokana na kuwa majeruhi, amesema watapambana wachukue makombe hayo baada ya kutupwa nje na UD do Songo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya awali kabisa.

Bocco ameliambia Championi Jumamosi kuwa, kwa sasa wanaweka mikakati ya kutwaa makombe hayo hasa la ligi ili wapate nafasi tena ya kurejea kwenye Ligi ya Mabingwa ambapo msimu uliopita walifika hatua ya robo fainali.

“Kweli tulikuwa na hali ya huzuni kwa wachezaji hasa baada ya kuondolewa mapema jambo ambalo hatukuwa tumelitarajia kabisa.

“Lakini kwa sasa tumepanga kuchukua mataji yote ili kupata nafasi ya kurejea tena kimataifa lakini pia kuwafurahisha mashabiki wetu baada ya kutokea kwa hali hiyo,” alisema Bocco ambaye ni mchezaji wa zamani wa Azam aliyejijenga na kuacha kivuli chake kwenye klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic