September 19, 2019


OBREY Chirwa, nyota wa zamani wa Yanga anayekipiga kwa sasa ndani ya Azam FC amesema kuwa yeye sio bishoo katika kazi kwani anajishughulisha pia na kilimo nje ya soka.

Chirwa ambaye kwa sasa ana kibarua kizito kuivusha Azam FC kwenye hatua ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho mbele ya Traingel United amesema kuwa wachezaji wa Tanzania hawapendi kujishugulisha.

 "Sehemu moja tu wachezaji wa Tanzania wanakosea, hawapendi kujiongeza na kufikiria maisha mengine nje ya soka, wengi wanapenda starehe na kufanya vitu ambavyo havina faida kwa maisha ya baadaye.

"Mimi sio bishoo na sina habari hizo kwani ninalima vizuri na kazi nyingine ninafanya kwa kujituma, mpira kwangu ni kipaji na ninamalengo nao," amesema Chirwa.


1 COMMENTS:

  1. Zesco 2 Yanga 0 mechi ya marudiano Ndola September 28, 2019

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic