September 28, 2019


Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amesifia kiwango cha mshambuliaji wa timu hiyo, Miraji Athuman 'Sheva' alichokionesha katika mechi za ligi alizozionesha ikiwemo dhidi ya Kagera Sugar.

Rage ameeleza kuwa Sheva ni moja ya wachezaji wazawa ambao wana viwango vizuri zaidi kuliko hata wanaosajiliwa kutokaa nje ya Tanzania.

Amefunguka kwa kumsifia kuwa endapo ataendelea kuzitendea haki dakika anazopewa na Kocha Patrick Aussems, itamsaidia kujijenga vizuri zaidi na kujitengenezea nafasi ya kupata timu nje ya Tanzania.

"Miraji ni mchezaji mzuri kwakweli, nimemtazama katika mechi zote alizocheza na kikosi cha Simba kwa msimu huu amekuwa na moto wa aina yake.

"Namshauri azidi kuzipigania dakika anazopewa na Kocha wake ili aweze kujitengenezea njia nzuri zaidi ya kwenda kucheza soka la kulipwa."

Kwa upande mwingine, Rage amefungu kwa kusifia namna Simba ilivyocheza mechi ya juzi dhidi ya Kagera na kusema wapinzani wao wana bahati maana ilikuwa wafungwe nane.

Ameeleza Kagera waliponea chupuchupu kutokana na namna Simba walivyosakata soka lakini bahati haikuwa yao haswa katika umaliziaji kulionekana mapungufu kidogo.


3 COMMENTS:

  1. Ila kocha alichelewa kumuingiza Miraji Athumani. Hizo goli nane anazosema Rage zimekosekana angalau tano sababu ni hiyo ya kocha kuchelewa kufanya sub.

    ReplyDelete
  2. Yule kijana sie wa kugaiwa dakika lakini wa kunyakuwa dakika zote tisini.

    ReplyDelete
  3. Acha azoee kwanza atapewa zote 90 muda wake utafika tuwe na subra.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic