NOEL Mwandila Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa kikosi kipo tayari kuwavaa wapinzani wao Zesco kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa leo nchini Zambia.
Yanga ina kibarua leo ugenini kupata matokeo mbele ya Zesco baada ya mchezo wa kwanza uwanja wa Taifa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 ili kusonga mbele wanalazimika kutafuta ushindi wa mabao zaidi ya mawili.
Mwandila amesema kuwa maandalizi ya kikosi yapo sawa na wanatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila watapambana kupata matokeo.
"Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu hilo lipo wazi na wachezaji tumewaambia kwamba tunahitaji ushindi hicho ndicho tunachokipigia hesabu kwa sasa mashabiki watupe sapoti," amesema.







0 COMMENTS:
Post a Comment