RAGE APINGANA KABISA NA HAJI MANARA, AUNGANA NA YANGA
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amewatawaka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuhakikisha wanaipa sapoti Yanga kuelekea mechi yao na Zesco United leo.
Yanga watakuwa na kibarua kizito kukipiga na miamba hao wa Zambia ambao tayari wameshawasili jijini Dar es Salaam tangu Jumatano iliyopita, katika mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Rage amesema suala la uzalendo ni muhimu kwa taifa letu sababu unatia hamasa haswa timu zinapocheza mashindano ya kimataifa.
Mwenyekiti huyo wa zamani amefunguka kwa kupingana na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ambaye amekuwa akihamasisha mashabiki wa timu yake waende kuishabikia Zesco kuwa si sahihi kufanya hivyo.
"Unajua linapokuja suala la uzalendo sote tunapaswa kuwa wamoja sababu itatutsaidia katika mashindano.
"Kwanza naomba ijulikane tu kuwa kama Yanga wakifanya vema kama ilivyokuwa kwa Simba msimu uliopita, tutakuwa na timu nne zitakazoshiriki mashindano kutoka Tanzania.
"Hakuna haja ya kwenda kuwazomea Yanga, sisi tunapaswa kuinyanyua bendera ya taifa letu, pale Taifa hatuna bendera ya Simba wala Yanga," alisema Rage.
Kwa upande mwingine, Rage amewaasa wachezaji wa Yanga kuhakikisha wanajiamini pindi watakapokuwa wanakabiliana na Zesco ili kupata morali ya kupata matokeo.
Amewataka ni vema wakacheza kwa mbinu za kufunguka na kulinda lango lao ili wasiruhusu kufungwa na vilevile wafanye vile wawezavyo waweze kupata bao la mapema ili kujitenegenezea mazingira ya kufunga mabao mengine zaidi.
Rage hana kauli ya kuwaambia wanasimba wakamsiliza zidi ya Manara. Mashabiki wa Simba kesho wataisapoti zesco .
ReplyDeleteSawa Mzee tumekusikia vizuri sana
ReplyDeleteWanaogopa yanga akishinda tuu mitaani hakuta pitika
ReplyDeleteNa Yanga wapo tayari kuipa sapoti Simba japo usoni tu na Moyni kwengine?
ReplyDeleteUnajua ukiwa unaoga akaja Mwehu kuchukua Taulo lako na kukimbia nalo na Wewe ukatoka Uchi na kumkimbiza, Watu wenye hekima Watakuona Wewe ulioko Uchi ni Mwehu na Mwehu kawa Mzima, tumemzoea huyo, Anatumiwa.
ReplyDeleteSasa hapo nani mwehu?
DeleteWe Rage hamia huko sisi usituchanganye waulize hao unaowasemea walifanya nini sisi tulipoondolewa tena bila kufungwa hiyo biashara ya usalendo haipo kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake wewe kawashangilie tu na hamia huko kabisaa usituchanganye.
ReplyDelete