MWINYI
Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amewatazama wapinzani wake wa leo kimataifa Zesco
kwenye mechi zao tatu ambazo ni sawa na dakika 270.
Yanga
inacheza leo na Zesco, uwanja wa Taifa ikiwa ipo chini ya Kocha Mkuu George
Lwandamina ambaye aliwahi kuionoa Yanga.
Zahera amesema kuwa alipata muda wa kuitazama timu ya
wapinzani wao Zesco kwenye michezo yao mitatu ambayo walicheza.
“Nawatambua
vizuri Zesco namna walivyo bora na udhaifu wao ulipojificha, nimewafuatilia kwa
ukaribu na nina imani ya kupata matokeo kutokana na maandalizi ambayo
tumefanya.
“Mechi tatu
ngumu kwao ilikuwa dhidi ya TP Mazembe ambao walicheza nao pia walicheza mechi
mbili na Zanaco zote nilizitazama sina mashaka na kikosi changeu tupo vizuri,”
amesema Zahera.
0 COMMENTS:
Post a Comment