SASA
kazi imenoga kwenye michuano ya Sprite Bball Kings 2019 baada ya timu mbili
kutinga fainali ya kuwania milioni kumi kwa mshindi wa kwanza kwa kushinda nusu
fainali zao mbili walizocheza.
Timu
ya Tamaduni ambayo iliibuka na ushindi wa vikapu 116 dhidi ya 65 vya KG Dallas
kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili huku Cornel Joseph akifunga pointi 28,
rebounds 10 na assist 1. Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali wikiendi
iliyopita, Tamaduni iliibuka na ushindi wa vikapu 99 dhidi ya 78 vya KG Dallas.
Mchenga Bball Stars iliibuka na ushindi wa
vikapu 105 dhidi ya 72 vya Flying Dribblers huku mchezaji, Baraka
Sadick wa Mchenga akifunga jumla ya pointi 49, rebounds 2 na assist 2.
Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali, Mchenga Bball Stars iliibuka na
ushindi wa vikapu 95 dhidi ya 71 vya Flying Dribblers.
Fainali
sasa itawakutanisha mabingwa watetezi Mchenga Bball Stars dhidi ya Tamaduni
ambao walishinda kwenye nusu fainali mbili walizocheza na sasa ikiwa ni msimu
wa tatu kwa michuano hii kufanyika.








0 COMMENTS:
Post a Comment